Duh! Mauzauza ya Hamisa na Diamond yateka mitandao ya kijamii!

Wednesday September 5 2018

 

By Rhobi Chacha

Kutokana na tuhuma za ushirikina  kwa mwanamitindo Hamisa Mobetto, kudaiwa kwenda kwa mganga kwa madai ya kumroga Diamond na mama yake ili wampende, mwanamitindo huyo amefunguka.

Akizungumza na MCL Digital Hamisa baada ya kuulizwa  tuhuma hizo,ambapo amesema, kama mengine yatapita basi na hili litapita akakata simu.

Mapema jana Diamond kupitia kipindi cha Refresh cha Wasafi TV alidai kwamba alitumiwa sauti ya mrembo huyo akizungumza na mganga wakiweka mikakati ya kuiroga familia yake na kuamini kuwa hiyo sauti ni ya Hamisa.

Baada ya hiyo Diamond amefunguka kuzungumzia sakata hilo  la kutaka kurogwa na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto ambapo alisikika akisema haya katika mahojiano hayo:

 “Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe,” alisema Diamond kupitia Refresh ya Wasafi TV.

Aliongeza,”Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi.”

 

 

Advertisement