Du! Ronaldo amvulia kofia Kylain Mbappe

Muktasari:

Ronaldo anayekipiga Juventus akiwa anaelekea mwishoni mwa enzi zake za soka anaamini Mbappe atafanya makubwa kwa muda mrefu a kwenye soka.

TURIN, ITALIA . CRISTIANO Ronaldo amemvulia kofia straika wa Paris Saint Germain, Kylian Mbappe kwa kukubali kuwa Mfaransa huyo ndiye staa wa soka wa sasa na miaka kibao mbele.

Katika video moja ya tangazo, Ronaldo anaonekana akimwagia sifa Mbappe kwa kusema: “Mbappe ni staa wa sasa na wa kizazi kijacho cha soka, ni mchezaji bora sana, ana kasi na atakuja kutawala katika siku za usoni.”

Ronaldo anayekipiga Juventus akiwa anaelekea mwishoni mwa enzi zake za soka anaamini Mbappe atafanya makubwa kwa muda mrefu a kwenye soka.

Tangu aibuke, Mbappe amekuwa akifanya makubwa kila kukicha na kuna kila dalili timu yake ya PSG inaweza kukutana na Juventus katika hatua zijazo za Ligi ya Mabingwa Ulaya, licha ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Borussia Dortmund katika mechi ya kwanza ya hatua ya 16 bora.