Drogba atundika daruga

Muktasari:

Drogba ambaye amestaafu akiwa na miaka 40, juzi alikuwa mzigoni  akiiongoza Phoenix Rising kwenye mchezo wa fainali ya kombe la USL ambapo aliishia kuambulia medali yake ya mwisho ya dhahabu.

MSHAMBULIAJI wa Kiavory Coast, Didier Drogba ametundika daruga rasmi kwenye soka huku akiambulia patupu baada ya timu yake ya His Phoenix Rising  kufungwa bao  1-0 na Louisville City.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea pia ni mmiliki wa klabu hiyo ambayo toka amejiunga nayo ameifungia jumla ya mabao 14 katika mashindano yote ndani ya michezo 22.

Drogba alifunga mabao 157 kwenye michezo 341 ambayo aliichezea Chelsea kati ya mika  2004 hadi  2012 na alifanikisha kushinda mataji matatu ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mshambuliaji huyo aliongeza taji lingine pindi aliporejea tena Chelsea msimu wa 2014-15, atokea kwa miamba ya soka ya Uturuki, Galatasaray.

Drogba ambaye pia aliichezea  Shanghai Shenhua ya China kabla ya kurejea Chelsea, alivyoondoka kwa mara nyingine  alijiunga na Montreal Impact ya Marekani kabla ya kumalizia soka kwenye timu yake.