Dk Tulia kuwasindikiza Simba kwa Waarabu Taifa

Muktasari:

  • Simba imepangwa kucheza Kundi D pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya Congo na JS Saoura.

Dar es Salaam. Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Ackson ataongoza maelfu ya mashabiki wa Simba na Tanzania kwa ujumla  kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria.
Simba klabu pekee inayowakilisha nchi na ukanda wa Afrika Mashariki katika hatua za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Tulia anakuwa mgeni rasmi wa kwanza kwenye hatua hiyo iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.
Mchezo huo, utapigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi majira ya saa 10:00.
Simba inaendelea na maandalizi yao kama kawaida tayari kwa mchezo huo.