Dk Tulia Ackson atwaa medali ya dhahabu

Muktasari:

Naibu Spika Dk Tulia Ackson imeendeleza ushindi wa ndugu zao wa soka, netiboli na wavu ( wanawake) baada ya kutwaa medali za dhahabu katika mchezo wa kutembea kwa haraka mbio mita mia nane (800m) na mbio mita mia nne kupokezana vijiti.

Timu ya mchezo wa riadha na kutembea (walkrace)  ya Bunge Sports Club ikiongozwa na Naibu Spika Dk Tulia Ackson imeendeleza ushindi wa ndugu zao wa soka, netiboli na wavu ( wanawake) baada ya kutwaa medali za dhahabu katika mchezo wa kutembea kwa haraka mbio mita mia nane (800m) na mbio mita mia nne kupokezana vijiti.
Alianza Dk Tulia ambaye aliibuka na dhahabu katika mashindano ya kutembea kwa haraka au maarufu mwendo kasi.
Agnes Marwa aliibuka mshindi wa pili baada ya kutwaa medali ya fedha.
Yosepher Haule alitetea medali yake ya dhahabu 800m  na Ana Gidarya aliyeshika nafasi ya tatu baada ya kutwaa medali ya shaba.
Kwa upande wa timu ya kupokezana vijiti (wanawake ) iliyoundwa na Waheshimiwa Rose Tweve, Yosepher Komba, Halima Mdee  na Zubeda Sakuru haikubakisha chochote baada ya kutwaa medali ya dhahabu.
Wanaume kupokezana vijiti  mita 400  (Relay) iliyoundwa na waheshimiwa  Shaban  Hassan Masala, Daniel Mtuka , Flatei Massay na  Alex Gashaza waliibuka washindi wa ya tatu baada ya kutwaa medali ya shaba.