Dk Mwakyembe azindua Jukwaa la Warusha Filamu na Maudhui

Muktasari:

Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Ramadhani Bukini  alitaja changamoto wanayokutana nayo ni kukosekana kwa vifaa bora na vyenye bei ya kueleweka kutokana na kuagizwa kutoka nchi za nje na kwa bei kubwa.

Dodoma.Waziri wa Habari ,Sanaa Michezo na Utamaduni Dk Harson Mwakyembe jana  alizindua   jukwaa la warushaji wa Filamu na Maudhui.
Dk. Mwakyembe alisema jukwaa hilo litawasaidia warushaji wa filamu na maudhui kufanya kazi zao vizuri na kuwa na mpangilio mzuri.
Dk. Mwakyembe alisema kuwa Novemba 28 hadi 30 kutakuwepo na tamasha la pamoja na mdahalo sambamba na uoneshaji wa filamu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Waziri alisema Watanzania wamekuwa wakichukulia filamu ni sehemu ya burudani badala ya kuelewa ni sekta mtambuka.
Hata hivyo alisema utengenezaji wa filamu  unahitaji weledi mpana ambao utakuwa na kiwango kizuri cha uelimishaji kwa jamii.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Isack Kamwelwe alisema Tanzania imekuwa kama sehemu ya kutupia vyuma chakavu kutokana na kuuziwa mitambo chakavu.
Kamwelwe alisema jukwaa la uandaaji na urushaji wa filamu na maudhuhi wakishirikiana kwa ukaribu wataweza kupata mitambo ambayo ni bora kwa lengo la kuboresha kazi za watengenezaji wa filamu nchini.
Katika hatua nyingine Kalwelwe alisema vituo vya kurusha habari kama havina vifaa vyenye ubora ni wazi kuwa hapawezekani kupatikana kwa habari na filamu zilizobora na badala yake itakuwa na vitu visivyo bora.
Mkurugenzi wa Jukwaa hilo Ramadhani Bukini  alitaja changamoto wanayokutana nayo ni kukosekana kwa vifaa bora na vyenye bei ya kueleweka kutokana na kuagizwa kutoka nchi za nje na kwa bei kubwa.