Djuma asepa kimyakimya

Muktasari:

  • Kocha msaidizi Mrundi, Masoud Djuma ameondoka nchini kimyakimya bila ya kutoa taarifa kama ilivyokuwa hapo awali.  Kwa mujibu wa Mratibu wa Simba, Abbas  Selemani, kocha huyo alitakiwa kuondoka mchana wa leo.

Dar es Salaam. Aliyekuwa kocha msaidizi wa Simba Mrundi, Masoud Djuma ameondoka nchini usiku wa manane kimyakimya.

Djuma aliondoka majira ya saa 9 usiku kimya kimya bila ya kupelekwa uwanja wa ndege na dereva wake kama ilivyokuwa utamaduni wa kocha huyo.

Mtu wangu karibu ambaye hakutaka jina lake liwekwe wazi alisema walikubaliana amfate leo (Jumatano) mchana lakini alishtuka asubuhi na kukutana na ujumbe wa kumuaga katika simu yake ya mkononi.

"Tulikubaliana nimfate mchana ili nimpeleke uwanjani wa ndege lakini naamka asubuhi nimekutana na ujumbe kuwa ameshaondoka tayari, " alisema.

"Nilipo jaribu kumpigia simu haikupatikana na mpaka sasa, " alisema.

"Ninacho fahamu Djuma alitakiwa kuondoka mchana wa leo zaidi ya hapo sina taarifa nyingine kama aliondoka usiku, " alisema Abbas Selemani Mratibu wa Simba.