Dimpozi: Simba sio ya Afrika

MSANII wa Bongo Fleva, Ommy Dimpozi  ambaye ni shabiki wa Simba amesema mafanikio inayopata klabu yake wanatakiwa kujifananisha na klabu kubwa za nje ya nchi.
Dimpozi alisema kwa upande wa nje ya uwanja uongozi unajitahidi kufanya mambo mazuri ya kuendeleza klabu yao hivyo wachezaji wanatakiwa kuweka nguvu uwanjani.
"Nataka kuiona Simba ikicheza klabu bingwa ya dunia huko mbele, tuna kila kitu hivi sasa na maendeleo yetu yameanza kuwa kama wao huko kwa wenzetu hivyo nadhani watu wa kujilinganisha nao ni wa huko Ulaya," alisema.
Dimpozi aliongeza kwa kusema kwamba suala la ushindi katika mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa Januari 4 mwakani sio jambo la kuzungumzia kwani linafahamika.
Kwa upande wa msanii, Mwana FA alisema Yanga wanatakiwa kuiga mafanikio ambayo wanayafanya na sio kuishia utani wa jadi kikawaida.
"Tusiwe tunataniana tu kwamba watani lakini hatuigani mazuri ambayo tunayafanya kwaajili ya mpira wetu, hivi ni vitu vikubwa na vinatakiwa kuigwa," alisema.