Dimpozi, Mwana FA wabariki mabadiliko ya Simba

Muktasari:

Wasanii Ommy Dimpozi na Mwana FA wamejitokeza katika uzinduzi wa kadi mpya za Simba huku wakiwataka Yanga nao kuiga mfano huo.

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz na Mwana FA wamebariki kitendo cha klabu ya Simba kuzindua mfumo mpya wa kadi za kielectronic kupitia benki  ya Equity huku wakiwataka watani zao wa jadi Yanga nao kuiga mafanikio hayo.
Mwana FA na Dimpoz  ambao ni mashabiki wakubwa wa Simba walikuwepo leo Jumamosi  katika uzinduzi wa kadi hizo za wanachama na mashabiki uliofanyika katika mabanda ya maonyesho sabasaba jijini Dar es Salaam.
Dimpozi amesema hatua ambayo Simba  wameipiga ni kubwa kwani wanazidi kwenda katika levo nyingine.
"Tunazidi kuwa wa tofauti mpaka hivi sasa kwasababu hapa walichokifanya ni kuwakutanisha wanachama wao na kupata pesa kupitia akaunti watakazofungua pia litaiwezesha klabu kuingiza kipato kupitia kwa wanachama na mashabiki wake," amesema Dimpoz.
 Wakati huohuo Mwana FA alisema wapinzani wao wakubwa  Yanga wanatakiwa waige mafanikio ya wenzao na sio  kuendeleza utani usio na faida.
"Tusiwe tunatania tu kwamba watani watani lakini hatuigani mambo ya maendeleo, hivi ni vitu vikubwa mno kwa maisha ya soka letu," amesema Mwana FA.
Pia uzinduzi huo ulihudhuriwa na mtangazaji mahiri Salama Jabir ambaye ni shabiki kindakindaki wa Simba.