Breaking News
 

Dili la kubadilishana Pogba na Dybala latajwa

Tuesday September 11 2018

 

MANCHESTER United ipo tayari kumtumia kiungo wake staa, Paul Pogba kama chambo cha kumnasa mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala ambaye anahitajika Old Trafford wakati huu Pogba akitamani kuondoka klabuni hapo.

Inajulikana Barcelona inaongoza katika mbio za Pogba lakini staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa yupo tayari pia kurudi Juventus na United inaona hiyo ni fursa tosha kwao kumtumia kama chambo cha kumnasa Dybala.

Uhusiano wa Pogba na Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho umedorora kwa sasa na kwa kupitia kwa wakala wake, Mino Raiola, staa huyo amekuwa akihusishwa kuondoka Old Trafford katika siku za karibuni.

Advertisement