Diamond kuoa mwaka huu?

Muktasari:

Baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Tanasha Donna, Diamond Platnumz aliwahi kusema kuwa mwanamke mpya atakayempata, atamuoa

Ujumbe wa meneja wa mwanamuziki, Diamond Platnumz, Sallam Sharaff 'Sallam SK' wa kumtakia heri ya kuzaliwa mama mzazi wa msanii huyo jana, umezua hisia mitandaoni kuwa huenda kiongozi huyo wa kundi la WCB ataoa mwaka huu.

Katika ujumbe huo alioundika jana Jumatatu Julai 7, 2020 Sallam SK alimmwagia sifa kedekede mama huyo wa Diamond huku akichomekea maneno ya yanayoashiria kuwa msanii huyo inawezekana yupo katika maandalizi ya kuoa.

Ujumbe huo ulioenda sambamba na picha ya mama Diamond ulisomeka hivi, "Ukizungumzia mama mwenye Dangote zake,heri ya kuzaliwa Bi Sandra.

"Mama mpokea mahari na mtoa mahari mwaka huu, nakutakia maisha mema na marefu Amin," ameandika Sallam.

Katika kupokea mahari imetafsiriwa tukio la kuolewa kwa mtoto wake wa kwanza hivi ambaye ni Dada wa Diamond ajulikanae kwa jina la Esma Platnumz.

Lakini kwa vile mama huyo amejaliwa watoto wawili, upande wa kutoa mahari umetafsiriwa kama unamlenga Diamond ambaye ni mtoto wake wa kiume.

Nani ataolewa na Diamond? Mimi na wewe hatujui, kwani ni hivi karibuni baada ya kuachana na mzazi mwenzie Tanasha Dona anayetokea pande za Kenya, aliapa kuwa mwanamke mwingine atakayeingia naye kwenye mahusiano atamuoa kabisa.

Baadhi ya mashabiki walikuwa na maswali akiwemo Suleimanmu22 aliandika"mama Dangote alipokea mahari za Queen na Esma, tuambie anatoa za nani, anazipeleka wapi mwaka huu mbona mafumbo au simba anaoa? ".

Iceboy tz aliandika "Kwenye kutoa mahari hapo bado aisee,maana kijana wake…"

Deleally aliandika "Hapo kwa mtoa mahari boss unawachanganya watu, watahaha kutafuta nani anaoa mwaka huu".