Diamond kunogesha tamasha la Sanaa na Tamaduni

Saturday September 21 2019

 

By THOMAS NG'ITU

MSANII wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kesho Jumapili atanogesha tamasha la Sanaa na Tamaduni (JAMAFEST) litakalofanyika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.  
Katika kuhakikisha ushiriki wake katika Tamasha hilo, Diamond amewaomba radhi mashabiki wake wa mkoani Iringa kutoshiriki nao kwenye sherehe iliyoandaliwa kufanyika leo Jumapili baada ya kumalizika kwa shoo yake leo Jumamosi.
"Kwa upendo wa Nchi yangu na heshima kubwa ya Waziri wangu Harrison Mwakyembe, Wizara na Baraza la Sanaa na Utamaduni, Jumapili hii nitakuwepo uwanja wa Taifa kwenye Tamasha la Sanaa na Tamaduni, hivyo baada ya kumaliza shoo yangu asubuhi nitatua Dar es Salaam kuhakikisha uwanja wa Taifa balaa linakuwa zito," aliandika.
Wasanii wengine ambao watakuwepo kwenye tamasha hilo la siku nane ni Barnaba na Aslay kwa upande wa Bongo Fleva huku upande wa Singeli ni Sholo Mwamba.
Diamond hayupo katika orodha ya wasanii waliopo katika tamasha hili lakini kesho yeye ndiye atakayefungua mbele ya wananchi wa Tanzania na nchi mbalimbali.
Tamasha hili limeanza Septemba 20 jana Ijumaa litamalizika Septemba 29 mwaka huu.

Advertisement