Deschamps kumsaidia Pogba kuhamia Madrid

Thursday May 23 2019

 

PARIS, UFARANSA.KOCHA wa Ufaransa, Didier Deschamps yupo tayari kumsaidia kiungo wa Manchester United, Paul Pogba kwenye mpango wa kutimkia Real Madrid kwenye dirisha dili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Pogba ambaye Deschamps amemtaja kwenye kikosi chake cha Ufaransa kitakachocheza mechi mbili za kufuzu Euro 2020, amekuwa akihusishwa na mpango wa kutimkia Bernabeu.

Siku za karibuni Pogba amekuwa akicheza chini ya kiwango, lakini jambo hilo halijawahi kuwa tatizo kwa Deschamps na kuamua kumjumuisha katika kikosi chake kwanza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Bolivia kisha kufuatia mechi za kufuzu Euro 2020 dhidi ya Uturuki na Andorra mwezi ujao.

Deschamps alisema: “Kushuka kiwango si kitu cha Paul peke yake. Kama ataniuliza kuhusu kuhamia Real Madrid, basi nitampa ushauri wangu.”

Kocha Deschamps ameendelea kuwa na imani kwa Pogba licha ya kuwapiga chini straika wa Alexandre Lacazette, beki wa Man City, Aymeric Laporte na fowadi wa Man United, Anthony Martial.

Kikosi cha Ufaransa ni makipa: Hugo Lloris, Benjamin Lecomte, Alphonse Areola, Mike Maignan. Mabeki:

Advertisement

Ferland Mendy, Lucas Digne, Clement Lenglet, Samuel Umtiti, Raphael Varane, Kurt Zouma, Léo Dubois ,Benjamin Pavard. Viungo: Pogba, Tanguy Ndombele, N’Golo Kante, Blaise Matuidi, Moussa Sissoko.

Washambuliaji: Olivier Giroud, Kylian Mbappe, Kingsley Coman, Antoine Griezmann, Florian Thauvin, Wissam Ben Yedder, Thomas Lemar.

Advertisement