Daraja la Kwanza, chungu kila kona

Muktasari:

Kundi B linaongozwa na Gwambina ambayo inahitaji alama tatu kujihakikishia kupanda Ligi Kuu, Kundi A, mtihani bado mgumu kwa Dodoma FC inayoongoza kundi hilo kwa utofauti wa mabao matano dhidi ya Ihefu SC zote zikiwa na pointi 39

 

Wakati ligi zikitarajia kuanza kuchezwa, huku Ligi Daraja la Kwanza (FDL) hali bado imekuwa ngumu kila kona.

Kabla ligi kusimama tayari timu 10 zilikuwa zimetimua makocha, Pamba iliachana na Muhibu Kanu, na Fredy Felix 'Minziro', Geita Gold (Salvatory Edward), Stand United (Eliakim Christopher).

Atuga Manyundo (Mashujaa FC), Charles Mwambona (Boma FC), Maka Mwalwisa (Mbeya Kwanza), Salhina Mjengwa (Ihefu FC), Bakari Malima (Rhino Rangers), John Tamba (Mawenzi Market).

Kocha wa Boma FC, Mhibu Kanu anasema kikubwa alichojifunza hadi sasa kwenye FDL ni ushindani wa timu pamoja na namba kwa wachezaji.

"Kama FDL ingekuwa na mdhamini kama Ligi Kuu basi hii ni ligi bora kwangu kuliko zote kwa sasa hapa Tanzania maana imekuwa na watu wengi ambayo wanaifuatilia, tatizo ni changamoto za uchumi," anasema Kanu.

Ligi itakapofunguliwa Pan African itacheza na Ihefu FC, Mlale itaikaribisha Dodoma FC, Majimaji na Njombe Mji, Iringa United na Friends Rangers, African Lyon na Boma FC, Mbeya Kwanza na Cosmopolitan.

Kundi B, Gipco atakipiga na Mawenzi Market, Rhino Rangers dhidi ya Stand United, Mashujaa FC atacheza na AFC, Transit Camp mbele ya Gwambina FC, Geita Gold na Sahare All Stars wakati Green Warriors dhidi ya Pamba FC.

Gwambina FC inahitaji alama tatu kujihakikishia kucheza Ligi Kuu, wakati Dodoma FC na Ihefu kai bado ngumu kutokana na kulingana alama, wote wakiwa na alama 39.

Kabla ya ligi kusimama matokeo ya mwisho ya ligi hiyo ilikuwa hivi. Dodoma FC iliicha 2-0 Njombe Mji,

Transit Camp iliichapa 1-0 Pamba FC, Geita Gold nayo iliifunga 3-1 Mawenzi Market, Mlale FC ilichapwa 2-0 Majimaji FC.

Arusha FC ikiwa nyumbani ililala 1-0 na Rhino Rangers, Ihefu FC ilishinda 3-0 kwa Boma FC, African Lyon 6-0 mbele ya Pan African, na Friends Rangers ililala 1-0 kwa Cosmopolitan.

Mashujaa iliichapa 2-1 Stand United, Iringa United iliifunga 2-1 Mbeya Kwanza, Gipco FC ilishinda 3-0 Sahare na Green Warriors ililala 0-2 Gwambina FC.