Dakika tisini kuamua hatima Kundi D la Simba

Muktasari:

 

  • Mchezo wa Simba na AS Vita utakuwa na msisimko kutokana na kiu ya timu hiyo kuandika historia kwenye mashindano hayo.

Mechi nane za Ligi ya Mabingwa Afrika zinatarajiwa kuchezwa siku moja ya Jumamosi ili kupata timu zitakazoshindano hayo hatua ya robo fainali.

Mechi za robo fainali zimepangwa kuanza Ijumaa ya Aprili 5, huku kundi gumu zaidi likitajwa kuwa ni Kundi D.

Mpaka dakika 90 zitakapomalizika ndipo zitaamua timu zitakazofuzu hatua ya robo fainali kutokana na uhalisia kwamba kila timu inayo nafasi ya kufuzu.

Mechi hizo zitawakutanisha Horoya FC dhidi ya Orkando Pirates.  Pia Club Africa watakuwa wanawakaribisha Ismaily.

Mtanange mwingine utawakutanisha TP Mazembe dhidi ya Club Sportif Constantinois, huku FC Platinum watakuwa wanaonyesha kibarua kigumu dhidi ya E.S.T.

Timu ya Lobi Stars watacheza na Asec Mimosas huku Wydad Athletic Club watacheza na Mamelodi Sundowns.

Al Ahly Sporting Club watatoana jasho na  Jeunesse Sporting de la Saoura huku mchezo wa Simba na AS Vita utakuwa na msisimko kutokana na kiu ya timu hiyo kutaka kuandika historia kwenye mashindano hayo mwaka huu.