DR Congo yataja 23 kwa Afcon, Kasongo atemwa

Wednesday June 12 2019

 

Cairo, Misri. Kocha DR Congo, Jean-Florent Ibenge Ikwange ametangaza kikosi chake cha wachezaji 23 tayari kwa Afcon 2019, huku akimtema mshambuliaji wa zamani wa Zamalek, Kabongo Kasongo.

DR Congo ipo kundi A pamoja na Misri pamoja na Uganda, na Zimbabwe, na mechi ya kwanza ya kundi hilo itachezwa Juni 21.

Kasongo aliyeitwa katika kikosi cha awali cha wachezaji 32 wa DR Congo ameshindwa kupenya katika kikosi cha mwisho kutokana na kuonyesha kiwango kidogo katika klabu yake ya Saudi, Al Wehda.

Kikosi cha DR Congo kinaundwa na wachezaji chipukizi akiwemo nyota kutoka West Ham, Arthur Masuaku, Cédric Bakambu (Beijing Guoan) na nyota wa Anderlecht, Yannick Bolasie.

Kikosi DR Congo:

Makipa: Parfait Mandanda (FC Dinamo Bucarest), Anthony Mossi (Chiasso), Ley Matampi (Al Nassr)

Advertisement

Mabeki: DJuma Shabani (Vita Club), Christian Luyindama  (Galatasaray), Arthur Masuaku (West Ham), Wilfried Abro (Mka  Ankaragucu), Glody Ngonda (Vita Club), Marcel Tisserand (Wolfsboug), Bobo Ungenda (Primiero di Agosto)

Viungo: Chadrac Akolo  (Stuttgart), Merveille Bokadi (Standard Liege), Chancel Mangulu (Porto), Paul Mpoku (Standard Liege), Tresor Mputu (TP Mazembe), Youssouf Mulumbu (Kilmarnock)

Washambuliaji: Britt Assombalanga (Middlesbrough), Cédric Bakambu (Beijing Guoan), Yannick Bolasie  (Anderlecht), Jonathan Mpangi (Antwerp),  Jackson Muleka (TP Mazembe).

Advertisement