Coutinho agombewa Ulaya

Muktasari:

Chelsea na Man United zimeonyesha nia ya kutaka kumrejesha Mbrazil huyo katika Ligi Kuu England

London, England.Chelsea, Paris Saint Germain na Manchester United zinamtolea macho mshambuliaji nyota wa Barcelona Philippe Coutinho zikitaka kumsajili majira ya kiangazi.

Coutinho amekuwa akihaha kurejea katika ubora wake baada ya kushindwa kutamba tangu alipojiunga na kigogo hicho mwaka jana akitokea Liverpool.

Chelsea na Man United zimeonyesha nia ya kutaka kumrejesha Mbrazil huyo katika Ligi Kuu England. (Dailymail)