Club Africain ya Tunisia yapewa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ismailia

Muktasari:

  • Mechi hiyon ya Kundi C ilivunjika wakati wa muda wa majeruhi baada ya mashabiki wa Ismailia kuanza kurusha chupa za maji uwanjani wakati timu yao ikiwa nyuma kwa mabao 2-1.


Club Africain ya Tunisia imepewa ushindi wa mabao 3-0 na wapinzani wao kutoka Misri, Ismailly imepigwa faini ya Euro 35,000 baada ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika kuvunjika.
Katika hatua zaidi, Ismaily italazimika kucheza mechi ijayo ya nyumbani dhidi ya CS Constantine ya Algeria Jumamosi, bila ya watazamaji.
Africain ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1 dhidi ya Ismaily 2-1 nchini Misri katika mechi hiyo iliyofanyika January 18 wakati chupa za maji zilipoanza kurushwa uwanjani, na kulazimisha waamuzi kuvunja mchezo huo wa Kundi C wakati wa muda wa nyongeza.
Ismaily ilikuwa imeondolewa kwenye michuano hiyo mikubwa ya klabu kabla ya rufaa yao kukubaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
CAF ilisema ilikubali rufaa hiyo kutokana na ukweli kwamba mashabiki hawakuvamia uwanja.
TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi nne wakati Ismaily haijaambulia chochote.
Ismaily na Constantine zimeshacheza mechi mbili kulinganisha na wapinzani wao na zitakutana Februari 23 na Mach 2 kufikisha idadi ya mechi za wenzao.
Uwanja ambao vurugu hizo zilitokea ni mmoja katika ya viwanja sita vitakavyotumika wakati wa fainali za Mataifa ya Afrika zitakazofanyika kuanzia Juni hadi Julai.
Misri imechukua nafasi ya Cameroon ambayo ilikuwa haijakamilisha maandalizi ya michuano hiyo mikubwa kwa timu za taifa.