Cioaba apata kibali

Kocha mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba anatarajiwa kurejea nchini siku chache zijazo baada ya kupata kibali cha kutoka nje ya nchi yake ya Romania.
Cioaba amekwama Romania alikorudi baada ya ligi kusimamishwa ili kuchukua tahadhari ya virusi vya Corona kutokana na sheria ya kutotoka nje kwa raia wa nchi hiyo na kufungwa kwa mipaka na viwanja vya ndege kwa wasafiri wanaotoka na kuingia kutoka nchi nyingine.
Ofisa habari wa Azam FC, Thabit Zakaria anasema juhudi za  muwakilishi wao nchini Romania zimesaidia kocha huyo kupatiwa kibali cha kusafiri kurudi nchini.
"Muwakilishi wetu ametupambania na kuhakikisha kocha wetu anapata kibali cha kuja nchini ambacho kimepatikana tayari.
Kwa hiyo kocha atasafiri kwa basi hadi nchi jirani ya Ujerumani ambako ndege zimeanza kuruka na hapo ataunganisha kuja Tanzania
Kwa maana hiyo muda wowote kuanzia wakati huu anaweza kuwasili nchini na kuendelea na majukumu yake," inasema Zakaria.