Chipukizi Yanga ajifunga Polisi Tanzania mwaka mmoja

Muktasari:

  • Msagati ni miongoni mwa nyota wa kikosi cha Yanga chenye umri chini ya miaka 20 kilicho maliza mashindano ya vijana kwa kuchukua mshindi namba tatu wakati ubingwa ulichukuliwa na Mtibwa Sugar na Azam alishika nafasi ya pili.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa timu ya vijana ya Yanga U20, Erick Msagati amejiunga mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Polisi Tanzania iliyopanda daraja msimu huu tayari kwa kukipiga Ligi Kuu.

Msagati alifanya vizuri katika mashindano ya ligi ya vijana chini ya umri wa miaka 20 yaliyomalizika hivi karibuni na Yanga kuchukua mshindi wa tatu baadaya kuwafunga Simba.

Msagati alisema anatarajia kukutana na changamoto mpya katika kikosi hicho kutokana na kutoka kushiriki ligi ya vijana na sasa anakutana na wakongwe na wazoefu wa Ligi Kuu.

"Nimelipokee hili kwa furaha na nilikuwa natamani sana kuona naingia katika changamoto kutokana na kuamini kama ninaweza kucheza soka lolote la ushindani naamini nitaweza kufanya vizuri endapo mwalimu ataniamini na kunipa nafasi,"

"Changamoto niliyonayo ni kuhakikisha namshawishi kocha ili aweze kunipa nafani na kuniamini kufanya kitu ambacho kitaibeba timu kwenye ligi hiyo ambayo inatarajia kuanza hivi karibuni."