Chelsea yampagawisha Kovacic

Friday August 10 2018

 

LONDON, ENGLAND. Kiungo Mateo Kovacic ameripotiwa kuwa na furaha kupita kiasi baada ya kuhamisha uhamisho wake wa kujiunga na Chelsea.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Croatia amekwenda kujiunga kwenye kikosi cha Chelsea kwa mkopo na hivyo atakuwa chini ya kocha Maurizio Sarri kwa msimu ujao.

Mkopo huo wa Kovacic ni sehemu ya dili la kipa Thibaut Courtois kwenda kujiunga na Real Madrid kwa ada ya Pauni 35 milioni.

Kovacic alisema: "Nina furaha kubwa sana kuwa hapa Chelsea. Ni jambo lenye hisia ya kipekee.

"Nitajitahidi kufanya kwa uwezo wangu kuisaidia klabu hii. Ni ligi mpya kwangu na siku zote mwanzo huwa mgumu, lakini nina hakika kocha na wachezaji wenzangu tutasaidiana, hivyo nasubiri msimu mpya uliobora."

Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia naye alisema: "Tunafuraha kumkaribisha Mateo kwenye familia ya Chelsea. Ni mchezaji anayefiti kwa msimu huu, staili yake ya kiuchezaji inaendana na anachotaka Maurizio na tunaamini atakuwa mtaji kwenye klabu yetu."

Advertisement