Chelsea yageuzia rada za usajili kwa Higuain

Wednesday January 9 2019

 

London, England. Chelsea inatarajiwa kuanza mazungumzo na mshambuliaji nguli wa AC Milan, Gonzalo Higuain ikitaka saini yake Januari, mwakani.

Kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amevutiwa na kiwango bora cha mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina katika kufunga mabao.

Higuain aliwahi kunolewa na Sarri katika msimu wa mwaka 2015-2016 alipokuwa kocha wa Napoli ya Italia.

Taarifa ya Sarri imekuja saa chache baada ya Chelsea kulala bao dhidi ya Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Kombe la FA uliochezwa juzi usiku.

Mshambuliaji huyo anacheza kwa mkopo AC Milan akitokea kwa ‘Kibibi Kizee’ cha Turin, Juventus.

Hata hivyo, Higuain mwenye miaka 31 amefunga mabao manane katika mechi 20 alizocheza AC Milan yenye maskani San Siro.

 

Advertisement