Chelsea,Man United vitani kisa Sancho

Muktasari:

Liverpool wao amejitoa kwenye mchakato wa kunasa saini ya Sancho, lakini wataketi tu pembeni kuona mambo yanavyokwenda katika vita ya kufukuzia saini ya mchezaji huyo. Hiyo ina maana vita hiyo itaahusu Man United na Chelsea.

LONDON,ENGLAND . BATO la wababe wawili. Manchester United na Chelsea watachuana jino kwa jino kwenye vita ya kumsajili Jadon Sancho, lakini si kwa dau la Pauni 100 milioni.

Borussia Dortmund wanajiandaa kukabiliana na vita kali na klabu vigogo wa Ulaya katika mpango wa kumbakiza staa wao huyo, hasa baada ya klabu mbili za Ligi Kuu England zikiingia kwenye vita kali kunasa saini yake.

Liverpool wao amejitoa kwenye mchakato wa kunasa saini ya Sancho, lakini wataketi tu pembeni kuona mambo yanavyokwenda katika vita ya kufukuzia saini ya mchezaji huyo. Hiyo ina maana vita hiyo itaahusu Man United na Chelsea.

Hata hivyo, hakuna timu hata moja itakayokuwa tayari kulipa pesa ndefu inayozidi Pauni 100 milioni baada ya sasa uchumi wa timu nyingi kuyumba kutokana na corona.

Beki wa zamani wa Man United, Rio Ferdinand alisema Man United itashinda katika mbio hizo za kumnasa Sancho, lakini kuna mambo wanayopasa kufanya hasa katika kutafuta nafasi ya kufuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.

Chelsea nao anahitaji saini ya mchezaji huyo, lakini wameweka wazi hawatweza kulipa mkwanja unaozidi Pauni 100 milioni kumsajili mchezaji huyo aliyecheza mechi 11 kwenye kikoi cha timu ya taifa ya England.

Kuhusu bei ndicho kitu ambacho Dortmund imeripotiwa itaking’ang’ania ili kuhakikisha mchezaji huyo anabaki kwenye kikosi chao. Real Madrid na vigogo wengine wa Ulaya akiwamo Bayern Munich nao ametajwa kufukuzia huduma yake.