Chambua: Watanzania tuhamasishane kuishangilia Serengeti Boys

Muktasari:

  • Watanzania wameombwa kila mmoja kwa nafasi yake ajitoe kuishangilia Serengeti Boys kwenye michuano ya AFCON inayoanza Aprili.

STAA wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kutoa hamasa kwa timu ya Serengeti Boys, kuelekea michuano ya AFCON itakayoanza Aprili mpaka 14 mpaka 28, Tanzania akiwa mwenyeji.

Chambua anasema Serengeti Boys ina uwezo wa kuandika historia katika michuano hiyo kwa madai wachezaji wanajituma na kuonyesha uwezo kwa mechi mbalimbali walizocheza.

"Hawa ni vijana wetu ambao wanaiwakilisha nchi, uwezo wanao lakini hata sisi lazima tuwahamasishe ili kuwaonyesha kwamba Watanzania tunawategemea.

"Kiufundi wanapaswa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, kujitolea muda wote watakaokuwa uwanjani, makocha wawajenge kujua ukubwa wa majukumu yao na kwamba wameibeba Tanzania mabegani mwao.

"Kitu chochote unapokifanya ukiona bendera ya Tanzania inasimamishwa basi ujue nikikubwa zaidi, hivyo vijana wetu wapewe motisha ya kuendelea kujituma kwa bidii, naamini watatufuta machozi na  kutufurahisha,"anasema.