Chama apagawa kwa ubingwa wa Ligi Kuu Bara

Thursday May 23 2019

 

By Eliya Solomon

Dar es Salaam. Kiungo wa Simba, Mzambia Clatous Chama amefurahia kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa katika msimu wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Chama alisema katika maisha yake ya soka amekuwa akipenda kucheza kwa mafanikio ndilo jambo atakalojivuania hata baada ya kuustafu.

“Nimefurahi kupata ubingwa huu, unamaana kubwa kwangu. Msimu huu umekuwa mzuri kwangu na kwa timu kwa ujumla na hata mashabiki wetu wameufurahia.

“Tulijitahidi kwa nguvu zetu kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa na tulipoishia tunaweza kuendelea msimu ujao kutokana na kutetea kwetu ubingwa wa ligi,” alisema Chama.

Chama alijiunga na Simba Juni 2 mwaka jana kwa kusaini mkataba wa miaka miwili utakaomalizika 2020.

Advertisement