Celine Dion hataki kufuatiliwa

Saturday February 2 2019

 

MWANAMAMA mwenye sauti tamu Celine Dion amevunja ukimya kuhusu maneno yanayoendelea dhidi ya mwonekano wake na kutaka aachwe kama alivyo.

Kauli hiyo ya Celine imekuja kutokana na maneno ya kejeli yanayotolewa dhidi yake namna anavyozidi kujikondesha na mavazi anayovaa.

Amedai anashangazwa na watu wanaozungumzia kuhusu mwili wake wakati yeye ndiye mwenye maamuzi afanye nini.

“Mwili ni wangu naamua vyovyote ninavyotaka na hata mavazi navaa kile ninachoona kinanifaa hivyo ningependa niachwe kama nilivyo,”

“Kama unanipenda niangalie jinsi nilivyo na kama hupendi mwonekano wangu niache angalia wengine,” alisema akihojiwa na Hollywood gossip.

Advertisement