CAF yaipiga bonge la busti ‘Kogalo Sirkal’

Muktasari:

Wikendi hii, Kogalo watarudiana na Waburundi Aigle Noir uwanjani Kasarani kwenye mechi ya kwanza ya mchujo kufuatia sare tasa waliyosajili ugenini.

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu (KPL) Gor Mahia ‘Kogalo Sirkal’ wamepigwa bonge la busti na CAF kwenye  harakati zao za kufuzu kushiriki dimba la Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Kogalo walikuwa wamefungiwa na CAF kuwatumia mastraika wawili wasiokuwa wazalendo, Mghana Francis Afriyie na Gislein Jikpe wa Ivory Coast baada ya kuchelewa kusajilisha majina yao na chombo hicho.

Hata hivyo, baada ya kuirai CAF iwaruhusu hatimaye ombi lao limekubaliwa na sasa wapo huru kuwatumia ila tu kuanzia kwenye mechi ijayo baada ya watakayocheza Jumapili hii.

Wikendi hii, Kogalo watarudiana na Waburundi Aigle Noir uwanjani Kasarani kwenye mechi ya kwanza ya mchujo kufuatia sare tasa waliyosajili ugenini.

“Tumepokea mawasiliano kutoka kwa CAf wakitupa ruhusa ya kuwatumiwa mastraika hao wawili ila baada ya mechi yetu ya Jumapili. Hii hakika ni busti kubwa sana kwetu,” akaeleza Katibu Mkuu wa Gor Ronald Ngala.

Mafowadi hao waliotua kuziba nafasi zao Mrwanda, Jacques Tuyisenge na Mrundi, Francis Mustapha hawakutumika kwenye sare ya ugenini kule Bunjumbura wikendi iliyopita kutokana na kikwazo hicho.