Burdani, soka Kipaji hapatoshi buana!

Muktasari:

Timu hiyo ya Ball Kipaji ambayo maskani yake ni Vingunguti ilimaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye Kundi E ambalo nafasi ya pili lilichukuliwa na Ninga FC.

BAADA ya shughuli ya Friends Rangers na UV Temeke jana Alhamisi, mbungi la Ndondo CUP hatua ya robo fainali leo Ijumaa linahamia kwenye Uwanja wa Bandari ambako kutakuwa na mchezo baina ya Burudani na Ball Kipaji.

Burudani ya Temeke, ilimaliza ikiwa nafasi ya pili kwenye Kundi B nyuma ya Friends Rangers na kwenye hatua ya 16 Bora iliiondoa Mlalakua Rangers kwa mabao 2-1. Kwa upande wa Ball Kipaji ambayo inaundwa na mastaa kama Shaban Kisiga, Abeid Kisiga na Ishara Juma ilipenya robo fainali baada ya kuichapa Maracana kwa mabao 3-1.

Timu hiyo ya Ball Kipaji ambayo maskani yake ni Vingunguti ilimaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye Kundi E ambalo nafasi ya pili lilichukuliwa na Ninga FC.

Baada ya mechi ya leo, kesho Jumamosi kutakuwa na mchezo mwingine wa robo fainali kati ya Ninga FC na Toroli Kombaini ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Bandari Temeke.