Buffon kurithi mikoba ya Casilas

Muktasari:

Buffon anaenda kurithi mikoba ya Iker Casilas ambaye ametakiwa kupumzika kucheza soka baada ya kusumbuliwa na matatizo ya moyo.

KIPA Gigi Buffon aliyekuwa anaichezea klabu ya Paris Saint German, anakaribia kujiunga na FC Porto aliyokuwa anaidakia Iker Casilas.
Buffon anaenda kurithi mikoba ya Casilas ambaye ametangaza kustaafu baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo ambao unadaiwa kushindwa kupokea damu ya kutosha kwa wakati.
Wakala wa Buffon, Silavano Martina alikiri kuwasiliana na watu wa klabu hiyo na mteja wake ameonyesha kuhitaji kucheza zaidi.
"Buffon anataka kucheza kwa mwaka mmoja zaidi na Porto ni miongoni mwa timu ambazo anazipenda, lakini ana watoto wanne hivyo wanahitaji kusafiri ni jambo analoliwazia," anasema.
Anasema mteja wake alicheza na Sergio Conceicao na ni vizuri akiwa kama kocha wake hivi sasa katika timu kubwa ambazo zina historia kubwa Ulaya.
Aliongeza ndani ya siku 10 mbeleni watatoa uamuzi wao juu ya hatima ya kipa huyo mkongwe.