Bruno Fernandes aitia hofu Man United

Manchester, England. Manchester United imeripotiwa kuwa katika wasiwasi juu ya presha kubwa aliyonayo kiungio mshambuliaji wao mpya, Bruno Fernandes.

Mchezaji huyo mwenye miaka 26, amekuwa nyota wa Old Trafford tangu alipojiunga na miamba hiyo akitokea Sporting Lisbon usajili wa Januari, alitolewa wakati wa mapumziko dhidi ya Tottenham kwa matatizo ya misuli.

gazeti la michezo la Ureno la O Jogo liliandika kuwa kiungo huyo wa Man United inahofia kuwa mchezaji wao ana mawazo kutokana na fedha zilizolipwa kwa ajili ya usajili wake.

Kikosi cha kocha Ole Gunnar Solskjaer kinafahamu kuwa kinahitaji kuwa na subira katika kuhitaji huduma ya mpiga penalti wao mahiri katika michezo yao ijayo.

Suala hilo linadaiwa kuwa ndilo pia lililochangia kwa Mashetani Wekundu kuongeza watu katika siku ya mwisho ya dirisha la usajili. Man United ilifanya usajili wa mshambuliaji Edinson Cavani.

Miamba hiyo pia ilimsajili beki wa kushoto, Alex Telles aliyetua Old Trafford akitokea Porto kwa ada ua uhamisho inayofikia Pauni 15.3 milioni.

Solskjaer pia alimsajili Amad Traore, Facundo Pellistri na Willy Kambala kikosini mwake. Sambamba na hao, Donny van de Beek alisajiliwa mapema.