Braithwaite atua barca kumrithi Dembele

Muktasari:

Baada ya wiki ya majadiliano hatimaye Barca iliamua kutoa dau la Euro 18 milioni ambalo lilikuwa kwenye mkataba wa straika huyo wa kimataifa wa Denmark anayetua Nou Camp kuziba pengo la Luis Suarez na Ousmane Dembele.

BARCELONA, HISPANIA . BARCELONA imeinasa saini ya straika wa Leganes, Martin Braithwaite kwa Euro 18 milioni ili kuziba pengo la Ousmane Dembele. Braithwaite amesaini mkataba ambao utamuweka Nou Camp hadi Juni 30, 2024, huku ukiwa na kipengele cha kuuzwa kwa dau la Euro 300 milioni.

Baada ya wiki ya majadiliano hatimaye Barca iliamua kutoa dau la Euro 18 milioni ambalo lilikuwa kwenye mkataba wa straika huyo wa kimataifa wa Denmark anayetua Nou Camp kuziba pengo la Luis Suarez na Ousmane Dembele.

Baada ya kupita Januari bila kusajili straika, Barca iliamua kurudi sokoni baada ya Dembele kuumia na chaguo la kwanza la timu hiyo lilikuwa Willian Jose wa Real Sociedad, lakini baada ya kumkosa ndipo walipomgeukia Braithwaite.