Bosi riadha aifagilia Simba

Monday June 29 2020

Simba ilijihakikishia rasmi taji hilo kwa mara tatu mfululizo baada kufikisha pointi 80 jana, ambazo hazitaweza kufikiwa na timu nyingine yoyote.
Akizungumza na Mwanaspoti, Nyambui alisema Simba wanastahili pongezi kwa kutwaa ubingwa lakini wanapaswa kujiandaa vyema ili wafanye vyema katika mashindano ya kimataifa msimu ujao
"Michezo yoyote inatawaliwa na uanamichezo. Mimi nikiwa mwanamichezo na kwa niaba ya wanamichezo wenzangu, naipongeza timu ya Simba, wachezaji wake pamoja na viongozi wa klabu kwa kuwa washindi wa ligi kuu katika msimu wa 2019/2020,"amesema Nyambui.
Katika hatua nyingine, Nyambui amewataka wachezaji wa Simba kujiandaa kimwili na kisaikolojia kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.
"Umoja ni nguvu utengano ni adui ya mafanikio, si mara ya kwanza Simba kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, nawaomba kusiwepo na visingizio," alisema Nyambui.
Kwa upande wao Simba kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari ya Klabu hiyo Haji Manara, wamewapongeza wachezaji na wanasimba wote kwa kuwa kitu kimoja katika kufanikisha kutwaa taji hilo.
Manara amesema kwa sasa wanasubiri wahusika kuwajulisha kombe lao watakabidhiwa katika mchezo gani kati ya saba iliyosalia kwenye Ligi Kuu.

 

Advertisement