Bongo Fleva wafurahia Ligi kurejea

Muktasari:

Msanii wa bongo fleva, Rashid Said'Bright' anaamini kurejea kwa Ligi Kuu Bara kutachangamsha vijiwe vya wanasoka,kubishana kuhusu Simba na Yanga.

MSANII wa bongo fleva, Rashid Said'Bright' amesema umefika wakati wa kuchangamsha vijiwe kwa kubishana kuhusiana na Simba na Yanga, Ligi Kuu Bara itakapoanza.

Bright ambaye ni shabiki wa Simba, amesema vijiwe vya soka vilipooza kutokana na kusimama kwa ligi, kutokana na uwepo wa ugonjwa wa covid 19, ambapo kwa sasa ameona furaha ya wanasoka itarejea.

"Ujue kuna vitu vinatufanya  tusahau kwa muda machungu ama ugumu wa maisha  kama soka, hivyo ligi inaporejea tutapata cha kubishana, vijiweni ama katika mitandao ya.kijamii"

"Amsha amsha za Simba na Yanga zinaleta afya za mioyo kwa mashabiki,huyu atacheka leo na yule atanuna kesho na  maisha yanaendelea,"amesema.

Bright ambaye anatamba na nyimbo yake mpya ya Adui amesema kukaa bila mikusanyiko ili kuepusha kusambaa kwa virusi vya corona, ilikuwa kama wapo kifungoni.

"Angalau kwa sasa tutatazama soka,tutasikiliza ama kufanya muziki na maisha mengine yataendelea,"amesema.