Bongo Flava, Hip Hop Bongo wapewa fursa

Thursday November 8 2018

 

By THOMAS NG'ITU

BOOM PLAY ni  huduma ya muziki inayoongoza upande wa kusikiliza na kupakua muziki na Universal Music Group (UMG), kampuni inayoongoza katika usambazaji wa muziki ulimwenguni, leo wanatangaza kusainiwa kwa makubaliano ya kibali cha kusambaza muziki katika masoko mengi ndani ya Afrika.
UMG ni kampuni ya kwanza ya muziki wa kupitisha leseni yake kwa Boomplay, ambayo inajulikana kwa huduma yake ya kusikiliza muziki barani Afrika. Chini ya makubaliano ya mkataba huu wa miaka mingi na ufanisi mara moja, Boomplay itasambaza muziki kutoka kwa UMG nchini Tanzania pamoja na Nigeria, Ghana, Kenya, Rwanda, Uganda na Zambia. Mpaka sasa, Boomplay ina nyimbo zaidi ya milioni mbili na maelfu ya video zinazopatikana kwa watumiaji wake zaidi ya milioni 36, na watumiaji karibu milioni mbili wanaoongezeka kila mwezi.
Katika hili, Makamu wa Rais wa Universal Music Group, idara ya Maendeleo ya Masoko, Adam Granite alisema, wanatarajia kuwawezesha wasanii wa Afrika kuongeza ubunifu ili kazi zao zizidi kukua.
 "Tunatarajia kufanya kazi na Boomplay ambapo tutawawezesha wasanii wetu wa Kiafrika kuwa wabunifu, jukwaa la masoko na uendelezaji wa rasilimali ili kuharakisha kazi zao zinaendelea kukua barani Afrika, lakini pia mkataba huu utasaidia wasanii wa UMG kufikia watumiaji wapya, huku wakiongeza hamasa ya usikilizaji wa muziki wa Afrika ili watapate faida kuwafikia mashabiki wa muziki, wasanii wengine na wazalishaji muziki". alisema.
Naye Meneja mkuu wa Universal Music, Ezegozie Eze Jr kutoka nchini Nigeria, alisema kuingia mkataba na kampuni hiyo wanatarajia kuona ubunifu kutoka kwa wasanij wa Africa.
"Ushirikiano huu utaendelea kufikia watu wengi na kuhakikisha kazi za wasanii wetu zinawafikia mamilioni ya wapenzi wa muziki barani Afrika," alisema.
Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Boomplay, Joe He, alisema kuwa Boomplay itaendelea kuunda ushirikiano unaoimarisha mfumo wa kidigitali na kuunganisha wapenzi wa muziki na nyimbo wananazozipenda wakati wowote na mahali popote.
“Boomplay imejizatiti kuendelea kutengeneza shauku kubwa ya muziki wa kiafrika katika njia halali, hasa kwa watumiaji wa Boomplay kushirikiana na lebo kubwa za muziki duniani kama Universal Music Group inatoa nafasi nyingine kubwa kwa sisi kufanya hivyo ", alisema.

Advertisement