Bondia Wilder amzimisha Breazeale sekunde 41 tu jukwaani

Sunday May 19 2019

 

Bondia Deontay Wilder amemtwanga kwa ‘knockout’ Dominic Breazeale katika raundi ya kwanza tu ya mpambano wao wa uzito wa juu  usiku wa kuamkia usiku wa kuamkia leo nchini Marekani.

 Wilder alifanikiwa kutetea taji hilo linalotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBC).

Kwa ushindi huo, Wilder ni kama ametuma salamu kwa bondioa Antony Joshua na Tyson Fury ambao ndio vinara wa taji la uzito wa juu nchini Marekani.

Bondia Breazeale alidumu jukwaa ni kwa sekunde 41 tu baada ya kutandikwa kombora ambalo lilimuweka chini kitendo ambacho kilimlazimu mwamuzi wa pambano hilo kumhesabia iwapo angeweza kuendelea na pambano.

 

Advertisement