Bonah atoa siri ya Wabunge Yanga

Muktasari:

Yanga wanacheza na Zesco United kutokea Zambia katika mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ua ule wa marudiano ambao utachezwa wiki moja inayofata.

MBUNGE wa jimbo la  Segerea (CCM), Bonnah Kamoli ni miongoni mwa watu maarufu ambao wamejitokeza uwanja wa taifa kushuhudia mechi ya Yanga dhidi ya Zesco United.
Bonnah alisema amekuja kuwakilisha Wabunge wote katika mchezo huo ambao wameshindwa kufika kutokana ratiba nyingine.
"Nimekuja hapa kuwawakilisha Wabunge wenzangu wa Yanga kwani tumekuwa tukiitakia kila la heri timu yetu katika kila mashindano.
"Siri kubwa ya Wabunge ambao tunaipenda Yanga tumekuwa tukiungana kuichangia hata katika kipindi kigumu cha kiuchumi ambacho kinapiti.
"Tumeunda kamati ndogo ya kuchangia ambayo hata mimi mwenyewr nipo kwani tunaimani kufanya vizuri kwa Yanga hata wananchi wetu wanasikia raha.
"Yanga ikishindwa kufanya vizuri huwa naumia, lakini naimani katika mchezo huu wa leo itafanya vizuri na tutashinda ili kuendeleza furaha ambayo tunayo sasa," alisema Bonnah.
Yanga wanacheza na Zesco United kutokea Zambia katika mchezo wa kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ua ule wa marudiano ambao utachezwa wiki moja inayofata.