Bocco tunaiheshimu African Lyon ila ushindi muhimu

Tuesday February 19 2019

 

By Bertha Ismail

Arusha. Nahodha wa Simba, John Rocco amesema wanatambua ugumu wa mchezo leo dhidi ya African Lyon hivyo wataingia kwa tahadhari kubwa ili kuvuna pointi tatu.
Bocco anatarajia kuongoza kikosi chake dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
"Kama tunavyosaka ushindi kutetea ubingwa ndivyo na wenzetu Lyon wanasaka ushindi kujiondoa mkiani hivyo tusipojiangalia na kuwa na tahadhari tunaweza kupoteza mchezo huu ambao ni muhim sana kwetu"
Bocco alisema kuwa katika mchezo wao atakaokosekana mchezaji Meddie Kagere hauwezi kuwa chanzo cha kupoteza mchezo huo kwani Simba kina wachezaji wengine.
"Simba ina wachezaji wengi tena wote ni wazuri tu hivyo kukosekana kwa Kagere hakuwezi kuwa na madhara sana kwani mtu yoyote atakayeaminiwa na kocha na kupewa nafasi tunaamini ataitendea haki nafasi hiyo."

Advertisement