Bocco awashusha presha Simba ubingwa Ligi Kuu

Muktasari:

  • Bocco anasema kuwa bado vita yao ya kuwania ubingwa ipo palepale na kwamba kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar haijaharibu chochote kwenye mipango yao.

Nahodha wa Simba, John Bocco amesema kuwa walipambana kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar  lakini wapinzani wao waliwazidi.

Hivyo matokeo hayo wanayasahau na sasa akili zao ni kwenye mechi ya leo Jumanne dhidi ya Alliance pale Kirumba Mwanza.

Amesema kuwa mashabiki wasikate tamaa kwani bado wana michezo mingi ambayo inaweza kuwapa nafasi ya kutetea taji lao la msimu huu hivyo waendelee kuisapoti Simba.

Anafafanua kuwa makosa waliyoyafanya benchi la ufundi limeona hivyo matumaini yao ni kuyafanyia kazi,huku wachezaji nao wakisikiliza maelekezo ili leo waweze kuibuka na pointi tatu.

“Tunajua mchezo ujao na Alliance (leo) utakuwa mgumu kwa sababu ni timu nzuri ambayo inahitaji ushindi,wamejiandaa kwa muda mrefu tofauti na sisi kwahiyo tutakuwa makini”anasema Bocco.

Nahodha huyo ameongeza kuwa bado vita yao ya kuwania ubingwa ipo palepale na kwamba kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar haijaharibu chochote kwenye mipango yao.