Bocco afikisha bao la 113, avunja rekodi yake Ligi Kuu

Thursday May 16 2019

 

By Thobias Sebastian

Mechi ya mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Simba wameibuka na udhidi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar huku John Bocco akiweka rekodi kwenye mchezo huo baada ya kufikisha bao la 113 kwenye maisha yake ya soka.

Bao hilo lilitokana na krosi iliyochongwa na mguu wa kushoto na Maddie Kagere kabla ya mfungaji Bocco kumalizia.

Bao hili linakuwa la 15 katika  msimu huu kwa Bocco ambaye atakuwa amevunja rekodi pia ya kufunga ya msimu uliopita.

Msimu uliopita Bocco alisajiliwa kuyokea Azam na ulikuwa msimu wake wa kwanza kucheza Simba.

Msimu huo Bocco alimaliza na ambao 14, ambayo msimu huu amevuka na kuvunja rekodi yake ya msimu uliopita.

Bacco anaweza kuongeza akaunti ya mabao kutokana Simba wamebakiwa na mechi nne kabla ya Ligi Kuu Bara kumalizika.

 

Advertisement