Bocco, Salamba waing'arisha Simba ikishinda mabao 3-0

Muktasari:

Dakika 27 Simba ilipata goli kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya Roland Msonjo kuunawa mpira kupitia krosi ya Pascal Wawa.

Timu ya Simba imeibuka na ushindi mnono kwa kuichapa African Lyon mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid leo Jumanne.

Mabao ya Simba yalifungwa na John Bocco (2) huku Peter Salamba akitupia wavuni bao moja.

Ushindi huo umeifanya Simba kufikisha alama 42 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikisalia nafasi ya tatu.

Katika mchezo huo Simba waliwaanzisha Aishi Manula, Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Paul Bukaba, Pascal Wawa, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Adam Salamba, john Bocco na Rashid Juma.

Kwenye  kikosi hiko ni nyota watatu tu ambao walioanza katika mchezo wa Ligi Kuu uliopita waliocheza dhidi ya Yanga, ambao ni Aish Manula, Pascal Wawa na John Bocco.

Katika kipindi cha kwanza timu zote zilikuwa zikicheza kwa kukamiana huku wakitumia spidi kupeleka mashambulizi yao kwa kuvizia langoni mwa mwenzake.

Simba walionekana kutaka goli la kuongoza lakini hata hivyo mipango yao iliokena kuwa hafifu kwani walishindwa kuipasua safu ya ulinzi ya African Lyon.

Dakika 18 Simba walipata kona na kupigwa kona fupi na Haruna Niyonzima, hata hivyo alipiga kona kupi kwa kuanzina na Nicholas Gyan ambaye alipiga shuti kali na kupaa.

Lyon waligeuka na kuanza kucheza mchezo wa kujilinda kwa kupaki basi, huku wakitumia mipira mirefu katika kupeleka mashambulizi licha ya kumsimamisha Stephen Mwasika katika eneo la ushambuliaji.

Dakika 27 Simba ilipata goli kupitia kwa John Bocco kwa mkwaju wa penalti baada ya Roland Msonjo kuunawa mpira kupitia krosi ya Pascal Wawa.

Wachezaji wa Lyon hawakuonyesha kulizika na maamuzi hayo na kumzonga muamuzi, lakini Muamuzi huyo hakuonyesha kutetereshwa na mizongo ya wachezaji hao.

Katika upande wa katikati kulikuwa na vuta ni kuvute ya nguvu kwa timu zote kiasi cha kufanya eneo hilo kutimua vumbi muda wote wa kipindi cha kwanza.

Viungo wa Lyon, Awadh Salum na Jabir Aziz waliweza kuwadhibiti vilivyo viungo wa Simba, Hassan Dilunga na Mzamiru Yassin

Dakika 44 Salamba alionyesha umahiri wa kutulia na mpira baada ya kupigwa krosi ndefu na Niyonzima na kuutuliza kwa kifua na kumpigia pasi John Bocco ambaye alikunjuka shuti kali na kipa kutema kwa haraka Salamba aliiandikia  Simba goli la pili.

Nicholas Gyan,Asante Kwasi,Bukaba Paul,Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga,Haruna Niyonzima,Adam Salamba, John Bocco na Rashid Juma.

Dakika 47 Simba ilipata goli la tatu baada ya kiungo mshambuliaji, Rashid Juma kukimbia na mpira kwa spidi upande wa kushoto na kupiga krosi ndani ya 18 na mpira huo ulimaliziwa vizuri na John Bocco.

Lyon walianza kwa nidhamu ya mchezo baada ya kucheza 4-5-1 lakini ghafla mfumo huo ulibadilika na ndipo Simba wakaanza kuutawala mchezo na kutupia mipira wavuni.

MOTOKEO MENGINE YA LIGI KUU KWENYE VIWANJA TOFAUTI

Mwadui 2-1 Biashara

Ruvu Shooting 0-0 Kagera

Coastal Union 1-1 Azam FC