Bocco: Mashabiki njooni kwa wingi AS Vita lazima afe

Friday March 15 2019

 

By CHARITY JAMES

NAHODHA wa Klabu ya Simba, John Bocco amewaita mashabiki wa kikosi hicho na Watanzania kwa ujumla kufika Uwanja wa Taifa kesho Jumamosi kwa wingi ili kushuhudia wanavyoandika historia kwa nchi na timu yao.


Bocco amesema hayo leo Ijumaa kuelekea mchezo wao dhidi ya AS Vita unaotarajia kuchezwa kesho Jumamosi majira ya saa 1:00  usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Amesema, wamefanya mazoezi kwa muda wa siku mbili tangu wapotua kutoka nchini Algeria hivyo wana molari kubwa ya ushindi kwa ajili ya kuweka historia hiyo.


"Tunacheza kwenye uwanja wa nyumbani. Tunacheza na klabu bora Afrika tunaiheshimu ni timu nzuri lakini ninachoamini tupo nyumbani pamoja na mashabiki wetu ambao ni wengi tu tunaowawakilisha,"alisema Bocco.


Akizungumzia kukosekana kwa kiungo, Jonas Mkude alisema timu yao ina wachezaji wengi na kila nafasi ina zaidi ya wawili hivyo atakaepata nafasi ya kucheza kesho atafanya vizuri.

Advertisement