Bizimungu afuta uteja wa Yanga, Azam

Muktasari:

Akizungumza na Gazeti hili alisema baada ya kupoteza michezo hiyo anajua anarejea tena jijini hapa kucheza michezo miwili, hivyo hataki kuondoka mikono mitupu.

Dar es Salaam. Kocha Ally Bizimungu wa Mwadui, amekiri kujipanga upya katika michezo yake ijayo ya ugenini, baada ya kupoteza hivi karibuni michezo yake miwili.

Bizimungu awali alipoteza dhidi ya Yanga baada ya kufungwa 3-1 kisha kupoteza dhidi ya Azam kwa kipigo cha 1-0 na kujikuta akipoteza michezo yote miwili ugenini.

Akizungumza na Gazeti hili alisema baada ya kupoteza michezo hiyo anajua anarejea tena jijini hapa kucheza michezo miwili, hivyo hataki kuondoka mikono mitupu.

“Tuna michezo miwili huko wiki ijayo sitaki tena kuja kizembe, nataka nihakikishe napata pointi ambazo zitaniweka kwenye msimamo vizuri kwasababu hayo ndio malengo yetu,” alisema.

Aliongeza kwamba timu yake imekuwa ikicheza soka safi na kupata matokeo katika michezo yake ya nyumbani, hivyo anahakikisha anapata njia sahihi ya kupata matokeo ugenini.

Mwadui watakuwa na kibarua ugenini dhidi ya JKT Tanzania Februari 1 na Simba Februari 7.