Biashara wao krosi tu, mabeki Yanga wajiangalie

Friday December 7 2018

 

By Thomas Ng'itu

KIKOSI cha Biashara United kikiwa kinaendelea na mazoezi katika uwanja wa Uhuru, mbinu

ambazo wameonekana kuzitumia sana ni mbinu za krosi.

Biashara katika mazoezi ya mbinu ambayo walikuwa wanafanya, kocha

msaidizi wa timu hii, Aman Josiah alikuwa akiwasisitiza mabeki wake wa pembeni kutulia na mpira kabla hawajapiga krosi.

Utulivu kwa mabeki hao wa pembeni ulianza kuonekana baada ya kusisitizwa kufanya hivyo na kocha huyo.

Mbinu ambazo wanatumia zitakuwa zinawalazimisha mabeki wa Yanga Haji Mwinyi na Paul Godfrey kutopanda mara kwa mara kwani wakifanya

hivyo watakuwa  wakiwapa upenyo Biashara kutengeneza mabao

 

 

 

Advertisement