Biashara United yaikomalia Yanga ikiifunga bao 1-0

Friday May 10 2019

 

Timu ya Yanga imeshindwa kufurukuta mbele ya Biashara United baada ya kupokea kipigio cha bao 1-0  mchezo wa Ligio Kuu kwenye Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Matokeo hayo, Simba imeendelea kubaki kileleni ikiwa na alama 81 huku Yanga wakiwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 80 kutokana na kupoteza michezo yao ya leo.

Dakika 50 Harritier Makambo nusura aiandikie bao la kuchomoa Yanga baada ya kuunganisha kwa kichwa faulo ya Thaban Kamusoko iliyotokana na Amis Tambwe kufanyiwa madhambi nje kidogo ya goli la Biashara Utd.

Hata hivyo Biashara nao walikuwa wakizidisha mashambulizi, dakika 53 winga George Makanga alikimbia kwa spidi kuelekea langoni mwa Yanga hata hivyo walijikuta wakigongana na beki Andrew Vicent na muamuzi alimpa kadi ya njano Vicent.

Katika kipindi cha kwanza timu zote zilianza kwa kushambuliana, Yanga walikuwa wakitumia mipira mirefu kupeleka mashambulizi, huku Biashara wakitumia mawinga wao katika kupeleka mashambulizi yao.

Ndani ya dakika nane aina ya mchezo iliyokuwa inatumika ni nguvu kwa timu zote mbili, huku kukiwa hakuna ufundi wowote ule katika dakika hizo za mwanzo.

Advertisement

 Biashara walipata goli la kwanza dakika 9 kupitia kwa mshambuliaji Tariq Kilakala baada ya kupokea krosi ya Wilfred Nkouluma huku mabeki wa Yanga wakijua ameotea na walishtukia mpira huo ukiwa wavuni.

Goli hilo liliwafanya Yanga waonekane kuamka na kutaka kupata goli la kuongoza lakini hata hivyo hali ya uwanja wa Karume (Mvua)  ilionekana kutokuwa rafiki kwa Mshambuliaji wao Herieter Makambo kwani mara kwa mara alikuwa akipteza mpira miguuni

Dakika 22 Makanga aliwachambua mabeki wa Yanga na kupiga shuti kali hata hivyo kipa Klaus Kindoki aliucheza mpira huo, safu ya ulinzi Yanga iliyokuwa na Andrew Vicent na Kelvin Yondan ilikuwa inakatika kutokana na kuwa na mawasiliano hafifu.

Dakika 38 Paul Godfrey alipewa kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi George Makanga alipokuwa anacheza mpira wa juu na kunyanyua mguu hali iliyofanya kuadhibiwa na muamuzi

Washambuliaji wa Biashara Utd Innoecent Edwin na Tariq Kilakala walikuwa wakitumia spidi kubwa katika kupenya safu ya ulinzi ya Yanga, spidi hiyo ilikuwa ikiwaendesha vilivyo Kelvin Yondani na Andrew Vicent.

Yanga kila waliopokuwa wanajaribu kupeleka mashambulizi langoni mwa Biashara, mabeki a timu hiyo walikuwa hawana cha kupoteza zaidi ya kuondoa hatari hizo kwa haraka (Kubutua).

Kipindi cha Pili Yanga walianza kwa spidi ya juu kwa kucheza pasi za haraka haraka, huku wakionekana wanahitaji kupata goli la kuchomoa katika mchezo huo.

Dakika 50 Makambo nusra aiandikie bao la kuchomoa Yanga baada ya kuonganisha kwa kichwa faulo ya Thaban Kamusoko iliyotokana na Amis Tambwe kufanyiwa madhambi nje kidogo ya goli la Biashara Utd.

Hata hivyo Biashara nao walikuwa wakizidisha mashambulizi, dakika 53 winga George Makanga alikimbia kwa spidi kuelekea langoni mwa Yanga hata hivyo walijikuta wakigongana na beki Andrew Vicent na muamuzi alimpa kadi ya njano Vicent.

Dakika 58 Yanga walifanya mabadiliko kwa kumtoa Rafael Daud na Mohammed Issa na nafasi zao zilichukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Mrisho Ngassa.

Baada ya kufanya mabadiliko hayo Yanga ilizidisha spidi ya kushambulia kutokana na uwezo wa Kaseke na Ngassa kuwa na spidi ya kupeleka mashambulizi.

Dakika 74 Yanga walitaka kupata goli kupitia Herieter Makambo baada Haji Mwinyi kupiga krosi katikati ya wachezaji na kugongana mpira ukaangukia miguuni mwa Makambo aliyepiga na kumbabatiza beki wa Biashara na kuwa kona isiyokuwa na faida.

Mchezo ulitawala mabavu kwa timu zote mbili, hilo lilitokana na wachezaji wa Biashara Utd kutumia nguvu nyingi katika kukaba wakati huo huo wachezaji wa Yanga nao wakitumia nguvu kwenye kushambulia.

Hali hiyo ilifanya ubabe nao kuibuka kwa wachezaji wa timu zote mbili kwa kila mmoja akiwa anatetea matokeo yake katika mchezo huo.

Dakika 81 Yanga walitaka kupata goli kupitia kwa Makambo baada ya kuonganisha krosi ya Haji Mwinyi, hata hivyo Kipa Abarola alitokea haraka na kuicheza krosi hiyo.

Kikosi cha Yanga, Klaus Kindoki , Paul Godfrey, mwinyi Haji, Andrew Vicent, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Mohammed Issa, Papy Tshishimbi, Herieter Makambo, Amis Tambwe na Raphael Daud.

Kikosi Biashara Utd, Nurdin Barola, Kauswa Benard,  Mpapi Nasibu, Wilfred Nkouluma, Lameck Chamkaga, Lenny Kisu, Juma Mpakala, Derick Kiakala, George Makanga na Inocent Edwin.

Advertisement