Ben Paul hana mchezo kabisa katika mapenzi

Muktasari:

Msanii wa Bongo Fleva, Ben Paul hana mzaha kabisa kwani baada ya kuachia nyimbo ya Ntala nawe kwa sasa amekuja na kibao kingine kinachozungumzia mapenzi pia ambacho ni Wakuone.

MSANII wa Bongo Fleva, Ben Paul ametoa kibao kipya kinachokwenda kwa jina la 'Wakuone' kinachozungumzia zaidi mapenzi kutokana na namna alivyozama kwa mwanamke mrembo anayempenda.
MCL Digital imezungumza na Ben Paul kama nyimbo hiyo inahusu maisha yake halisi hasa madai ya kuwa na mpenzi Mkenya ambaye ndiye habari ya mjini.
"Ni kweli kuna uhusiano kuhusu nyimbo hii ya Wakuone kwani inaweza kumhusu mtu yeyote nikiwemo mimi niliye katika mapenzi,"alisema Ben Paul
"Ujumbe wangu ni halisi kwa binadamu wa aina yeyote ambaye yuko katika mahusiano, kuna wakati unaweza kuyafurahia mapenzi ingawa kuna wakati yanaweza kugeuka na kuwa maumivu makali,"anasema.