Beki wa Yanga afiwa na mama yake aondoka kambini -VIDEO

Muktasari:

Hadi sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika uwanja wa Kirumba kujiandaa na mechi zake mbalimbali.

Mwanza. Simanzi imetawala katika mazoezi ya Yanga baada ya taarifa ya kufikiwa na mama yake nahodha msaidizi, Juma Abdul asubuhi ya leo Alhamisi Septemba 5.

Yanga ipo kambini jijini Mwanza tangu jana Jumatano, Abdul alikuwa miongoni mwa wachezaji waliopo kikosini kwa ajili ya kambi yao ya kujiandaa na mashindano yao mbalimbali.

Makamu Mwenyekiti wa Mashindano ya Klabu hiyo, Saady Khimji amethibitisha kutokea kifo hicho, huku akieleza kuwa tayari uongozi umeshafanya taratibu za mchezaji wao kusafiri kwa ajili ya kumzika mzazi wake.

"Hili ni pigo kubwa kwetu sote na tayari tumewasiliana na viongozi wa juu huko Dar es Salaam akiwamo Mwenyekiti Dk Mshindo Msola kuhakikisha tunashirikiana naye katika kipindi hiki kigumu, sisi huku Mwanza tumekamilisha suala la usafiri kwa Abdul ili aende kushiriki mazishi ya mzazi wake" alisema kiongozi huyo wa msafara.