Beki wa Majimaji apewa jina matata mtaani Dar

Wednesday December 6 2017

 

Beki wa Majimaji, Tumba Sued ameambulia kubatizwa jina la mtaani maeneo ya Magomeni Kagera na kamwe hutasikia mchezaji huyo akiitwa kwa jina lake.
Tumba ni maarufu zaidi kwa jina la utani la Mdudu Kiwi na mtaani kwao wote wanamfahamu kwa hilo. Alipachikwa jina hilo na jamaa zake wa karibu akiwemo kocha aliyemfundusha soka ambaye pia ni bosi wa Friends Rangers, Herry Mzozo kwa sababu ya rangi ya mwili wake ni nyeusi sana.
Tumba mwenyewe amekiri kuwa, hana shida kabisa na jina hilo kwa sababu limeshakuwa marufu na ni la kipekee na ndio A.K.A yake.
Beki huyo aliyetamba na klabu za Azam, Ashanti United na Mbeya City kwa sasa anakipiga Majimaji Songea.