Beki Yanga amtaka Kagere

Muktasari:

David Luhende amemchambua Meddie Kagere kwamba umarufu alionao kwa sasa sio kama alivyokuwa na timu ya Gor Mahia kwa madai uwingi wa mashabiki wa Simba ndio unaomfanya ajulikane kile sehemu.

Beki wa zamani wa Yanga, David Luhende ambaye kwa sasa anacheza Kagera Sugar, alisema Kagere awashukuru Simba wanaopaisha jina lake lakini anachokifanya dimbani ni sawa na mafowadi wa timu nyingine akimtolea mfano Edward Christopher na Msuva.
"Nikuambie kitu hata hao kina Marcel Kaheza, Mo Rashid na Adam Salamba wakifunga mechi nne mfululizo watageuka habari za mjini na huyo Kagere aombe Mungu aendelee kumsaidia kufunga hivyo hivyo.
"Kibongo bongo labda mchezaji pekee ambaye anatuonyesha ana kitu tofauti hata akiitwa timu ya Taifa Stars ni Mbwana Samatta kwa kuwa anakocheza Genk hakuna uswahili kama Bongo, kule ni kazi huyo hata beki naweza nikamuona ana kitu cha kipekee na sio hao wengine ni kawaida tu bali ni porojo,"alisema Luhende.

MABAO mawili aliyoyafunga Meddie Kagere, Simba ilipocheza na Coastal Union ya Tanga na ile hat- trick ya Emmanuel Okwi dhidi ya Ruvu Shooting, walionekana wao ndio habari ya mjini, jambo lililowaibua mabeki wanaokipiga ligi kuu na kutoa mitazamo yao juu ya  mastaa hao.
Ali Ali ni beki wa KMC alisema ni kweli Okwi na Kagere wana uwezo wa juu, huku akidai sifa zingine wanazidishiwa na mashabiki wao wasioangalia ufundi zaidi.
"Kusema ukweli huwezi kusema Okwi ni mbaya wakati msimu uliopita yeye ndiye alikuwa mfungaji bora, sema wakati mwingine mashabiki wanazidisha sifa, kuna vitu anavifanya Okwi vinafanana na alivyovifanya James Msuva, lakini kwa kuwa huyu yupo KMC hatavuma," alisema Ali.