Bayern Munich na kibarua kizito Bundersliga

Muktasari:

Bayern Munich ambao hawakufanya vizuri sana mzunguko wa kwanza wana nafasi ya kusahihisha makosa na kuanza kuwafukuzia Borussia Dortmund wanaoongoza ligi kwa sasa.

MZUNGUKO wa pili wa ligi ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, unatarajiwa kuanza wakati huohuo ukiwa ndio mzunguko wa lala salama huku timu zilizofanya vibaya katika mzunguko wa kwanza zikijipanga kufanya vyema.
Bayern Munich ambao hawakufanya vizuri sana mzunguko wa kwanza wana nafasi ya kusahihisha makosa na kuanza kuwafukuzia Borussia Dortmund wanaoongoza ligi kwa sasa.
Munich watakuwa ugenini kwa Hoffeiheim, ijumaa kwenye mchezo utakaopigwa saa 4:30 Usiku majira ya Afrika Mashariki na kuonyeshwa Mubashara kupitia ST World Football.
Kocha wa Dortmund Lucian Fevre alisema nyota wake Marco Reus aliyekuwa anasumbuliwa na tumbo na kinara wa magoli Bundesliga, Paco Alcacer aliyekuwa anasumbuliwa na nyama za paja wako fiti kucheza mchezo wa jumamosi.
Kwa upande wa RB Leipzig wao watawategemea zaidi Timo Werner mwenye kasi zaidi na Mshambuliaji wa Denmark mwenye asili ya Tanzania, Yussuf Poulsen ambaye ana nguvu za kutosha kuwasumbua mabeki wa kati wa Dortmund Dani Axel Zagadou na Manuel Akanji.
Bayer Leverkusen watawakaribisha Borussia Mochengladbach jumamosi saa 11:30 jioni na mchezo utakuwa LIVE kupitia ST World Football. Wapenzi wa Soka nchini wataweza kutazama mechi hizi kupitia StarTimes pekee kwa kulipia kifurushi cha MAMBO Tsh 14,000 (watumiaji wa Antenna) na SMART Tsh 21,000 (watumiaji wa Dish)