Batshuayi arejeshwa Chelsea

Thursday January 10 2019

 

VALENCIA, Hispania
Dar es Salaam. Klabu ya Valencia, imetangaza kusitishia dili la mkopo la mshambuliaji Michy Batshuayi.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji aliyeichezea pia Borussia Dotmund kwa mkopo msimu uliopita, ameshindwa kutamba Hispania tangu atue La Liga na Valencia imeamua kurejesha klabu yake Chelsea ya England.
Katika mechi 15 za La Liga, Batshuayi amefunga bao moja tu na Mkurungezi wa Michezo wa klabu huyo, Mateu Alemany alisema dili ya mchezaji huyo kukipiga kwao litafikia kikomo mwishoni mwa mwezi huu.
Akizungumza na wahabari mapema leo Alhamisi, Alemany alisema; "Mchezaji anajua kwamba ataondoka klabu na tunaimani kila kitu kitaenda sawa kwa panmde zote tatu zilizohusika kwenye dili hili."

Advertisement